DROGBA AREJEA KUHANGAISHA ARSENAL
Drogba arejea kuhangaisha Arsenal
05 Aug 2013 13:24:06
Didier Drogba alirejea kuwahangaisha Arsenal huku
mshambuliaji huyo wa Ivory Coast akifungia
Galatasaray mabao yote mawili kuwapa ushindi wa
2-1 katika Kombe la Emirates mnamo Jumapili.
Drogba alikuwa na mazoea ya kufunga vijana hao wa
Arsene Wenger alipokuwa Chelsea na, baada ya kuingia
kutoka benchi baada ya muda wa mapumziko,
makombora yake yalibatilisha bao la Theo Walcott la
kipindi cha kwanza na kuhakikisha timu hiyo ya
Uturuki inatoroka na ushindi wa dimba hilo la kirafiki
la kabla ya msimu ambalo lilishirikisha timu nne.
Vijana wa Wenger waliadhibiwa katika uwanja wao wa
Emirates kwa kukosa kutumia vyema presha
waliyoweka mapema kwa wapinzani wao na mchango
wa Drogba ulidhihirisha ni kwa nini Wenger anajaribu
sana kuongeza straika wa Liverpool Luis Suarez
kwenye kikosi chake.
Huku juhudi zake za kumnasa Suarez kufikia sasa
zikiwa zimefeli licha ya Arsenal kuwasilisha ofa ya £40
milioni kwa raia huyo wa Uruguay, mshambuliaji wa
Ufaransa wa timu isiyozidi umri wa miaka 20 Yaya
Sanogo kwa sasa ndiye tu aliyeongezwa kwenye kikosi
cha Wenger kabla ya msimu.....endelea
Comments
Post a Comment